Makamu wa Pili wa Rais Alhajj Hemed Abdulla amejumuika na waumini katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amejumuika na waumini wa Masjid Riyaadh Amani katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.Akiwasalimia waumini hao Alhajj Hemed amewataka wananchi kushirikiana na Serikali katika kupinga vitendo viovu nchini ambavyo vinamchukiza Allah (S.W) na kuondoa taswira ya Zanzibar. Amesema zipo njia nyingi zinazopelekea kuongezeka kwa vitendo hivyo